У нас вы можете посмотреть бесплатно AJALI YASABABISHA KIFO CHA MCHIMBAJI MMOJA, KATIKA MACHIMBO YA MWAKITOLYO NA.5 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mnamo tarehe 17/7/2020 kulitokea ajali iliyosababisha kifo cha mchimbaji mmoja katika kitalu cha Wachimbaji wadogo wa Namba 5 Kata ya mwakitolyo Wilayani Shinyanga. akiongea na Wachimbaji hao Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga Mha. Joseph Kumburu aliwataarifu kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 6 mchana wakati wachimbaji Wachimbaji zaidi ya watano walipokuwa wakitoka ndani ya Duara baada ya kumaliza kazi katika Duara 56D. Alieleza kuwa duara hilo lilikuwa na urefu wa zaidi ya mita 20 ambapo Marehemu alitambuliwa kwa jina la Michael T. Salumu (30), Mkazi wa Kijiji cha Masungura, Wilaya ya Meatu Afisa Madini huyo aliwataarifu kuwa Sababu zilitokana na marehemu kuanguka ndani ya duara baada kukosa nguvu na kupasuka kichwa wakati. Hata hivyo, Mtaalam wa Afya aliyekuwa kwenye uchunguzi huo, alitoa taarifa kuwa marehemu alipasuka kichwani na kusababisha umauti kutokana na kuanguka kutoka umbali mkubwa, Aidha alieleza kuwa marehemu hakuwa na majeraha yoyote zaidi ya kupasuka kichwa na kuwashauri Wachimbaji wadogo kuhakikisha wanazingatia Sheria za uchimbaji na maelekezo wanayopewa na Wataalam wa Madini na Jeshi la Polisi. Kutokana na matatizo ya ajali za Mara kwa Mara, katika machimbo ya mwakitolyo, Afisa Madini Kumburu alitangaza kufunga machimbo hayo kwa siku tatu kupisha ukaguzi maalum wa maduara yaliopo katika leseni 23 za Wachimbaji wadogo. Kusitishwa kwa uchimbaji kutafanyika kwa awamu kuanzia na leseni za eneo la Namba 5 na kufuatia leseni nyingine za Na4 hadi 1. Aidha, ili kufanikisha kazi hiyo, Afisa Madini huyo amenda Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Madini, Jeshi la Polisi Salawe na Ofisi ya Mkurugenzi kusimamia zoezi la ukaguzi na kushauri hatua za haraka za kuchukua kwa maduara yote yatakayobainika kuwa ni hatari kwa afya, Usalama na utunzaji wa mazingira. Pamoja na hilo, Afisa Madini aliwataka Wachimbaji hao kuhakikisha wanazingatia Sheria za Madini na maelekezo wanayopewa na wakaguzi sambamba na kufukia mashimo yote ambayo yameachwa wazi bila kufukiwa.