У нас вы можете посмотреть бесплатно #BREAKING или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbeya, Juni 8, 2025 – Watu 28 wamefariki dunia papo hapo na wengine 9 kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha lori lenye shehena ya unga wa ngano lililokuwa likielekea nchini Zambia kutoka Dar es Salaam. Ajali hiyo imetokea katika mtelemko mkali wa Mlima Mbalizi, mkoani Mbeya, baada ya lori hilo kufeli breki na kugonga magari mawili, likiwemo daladala la abiria, kabla ya magari hayo kutumbukia katika korongo la Mto Mbalizi. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, amesema juhudi za uokoaji zilianza mara moja kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya usalama na wakazi wa eneo hilo. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Juma Homera, alifika eneo la tukio na kueleza masikitiko yake kutokana na ajali hiyo, huku akitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.