У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MACHA AZINDUA SAMIA ARDHI KLINIKI,ATOA WITO KWA WANANCHI KUTUMIA FURSA HIYO MUHIMU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua Kliniki Maalumu ya Wanawake ijulikanayo kama “Samia Ardhi Kliniki” mkoani Simiyu, ikiwa ni jitihada za kuongeza umiliki wa ardhi kwa wanawake na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi. Akizindua kliniki hiyo Machi 4, 2026 mjini Bariadi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, alisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka kusaidia wanawake kumiliki ardhi kisheria. “Tunawahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kupata elimu, ushauri na huduma za kupimiwa maeneo pamoja na hati miliki,” alisema Macha. Takwimu za serikali zinaonesha kuwa ni takribani asilimia 28 pekee ya wanawake nchini wenye hati miliki, licha ya uwepo wa sera na sheria zinazolinda haki zao za kumiliki ardhi. Akitoa taarifa ya utekelezaji, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Simiyu, Denis Masami, alisema hadi Machi 4, 2026 jumla ya hati 198 zilikuwa zimetolewa kupitia kliniki hiyo, inayotarajiwa kuhitimishwa Machi 7 kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8. Alisema mkoa una lengo la kutoa hati 3,000 kwa mwaka 2025/2026, ambapo hadi sasa hati 1,441 zimetolewa, zikiwemo 403 za wanawake sawa na asilimia 28.