У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 12/03/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 12/03/2026 MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 20 NENO KUU: Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; MADA: "KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON) UJUMBE WA LEO: NAMNA NYAKATI NGUMU KWENYE MISIMU ZINAVYOWEZA KUTENGENEZA WATU WA KUSUDI. 3. Fikra zisizoogopa kushindwa bali zinaogopa kwenye kutojaribu. Moja ya Nyakati ngumu au misimu mibaya kwenye maisha ya mwanadamu ni majira ya kushindwa yaani kufeli mtihani, kushindwa kwenye michezo, uchaguzi, kushindwa kwenye ubunifu fulani nk. Ni muhimu uelewe kwamba njia ya kuelekea kwenye kusudi inaweza kuwa na kushindwa kwingi sana, zifundishe fikra zako zisiogope kule kushindwa bali ziogope kutojaribu kitu kipya maana huko ndiko kushindwa halisi. Mithali 24:16 MAMBO YANAYOSABABISHA MTU WA KUSUDI KUSHINDWA MARA NYINGI KABLA YA KUFIKIA KUSUDI. a. Ulimwengu wa roho unaweza kuona kufikiwa kwa kusudi fulani ndani ya mtu, hivyo unaongeza vita. Ile vita ndio inayosababisha kushindwa kabla ya kufikia kusudi. Mfano 1. Vita ya Danieli iliongezeka pale tu alipokaribia kupewa uwaziri mkuu enzi za Dario, na hii ikasababisha kutupwa kwenye tundu la simba. Danieli 6:1-3 Mfano 2. Ulimwengu wa roho ulipoona kufikiwa kwa kusudi kubwa la kuukomboa Ulimwengu uliinua vita na kuwaua watoto wa kiume wakati wa kuzaliwa kwa Yesu. Mathayo 2:16 Herode aliamua kuwa adui wa Yesu kwasababu Ulimwengu wa roho ulikuwa unazuia kusudi kubwa la ukombozi kwa Ulimwengu. Ufunuo 12:1-5 b. Kuzungukwa na watu wasiotamani ufike kwenye kusudi. Mwanzo 31:7 Yakobo alianguka/ alishindwa kwenye uwekezaji mara kumi kwasababu ya Labani aliyetaka Yakobo asifanikiwe, lakini aliinuka tena na akafika kwenye kusudi na kuwa matuo mawili. ▶️ Yusufu alianguka / alishindwa mara nyingi kabla ya kufika kwenye kusudi kwasababu ya ndugu zake Mwanzo 37:8 Kilichomchelewesha Yusufu kwenda kwenye kusudi na akaanguka mara nyingi kwa kutupwa kisimani, kuuzwa, na kufungwa ni kwasababu ya ndugu zake (watu waliomzunguka). Mtu wa kusudi lazima aelewe kwamba hata kama atakutana na watu watakaomfanyia ubaya ili aanguke, Mungu atautumia ubaya wao kumpeleka kwenye kusudi. Mwanzo 50:20 Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Matendo 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; Mhubiri: Mwl. Andrew Bartimayo Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com