У нас вы можете посмотреть бесплатно HATARI🔥TANESCO YALAUMIWA KUHATARISHA MAISHA YA FAMILIA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkazi mmoja wa Mtaa wa Majengo, Kata ya Bethrehemu, Mbinga Mjini mkoani Ruvuma,Amelilalamikia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mbinga kwa madai ya kutumia nyumba yake kama nguzo ya kupitishia waya wa umeme kwa ajili ya kumpelekea huduma jirani yake. Mkazi huyo amesema kuwa tukio hilo lilifanyika kabla nyumba yake haijaezekwa, ambapo TANESCO walipitisha waya wa umeme juu ya kuta za nyumba yake bila ridhaa yake. Ameeleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiomba waya huo uondolewe, lakini maombi yake yamekuwa yakipuuzwa bila kuchukuliwa hatua. Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wakati wa masika, mkazi huyo alilazimika kuezeka nyumba yake kwa hofu ya kuta kuharibika au kuanguka. Hata hivyo, hatua hiyo imesababisha waya wa umeme kubaki ukiwa ndani ya paa la nyumba hiyo, hali ambayo ni hatari kwa usalama wa familia yake na mali zao. Mkazi huyo anaiomba TANESCO Mbinga kuchukua hatua za haraka kuondoa waya huo ili kuzuia hatari inayoweza kujitokeza, ikiwemo majanga ya moto au ajali za umeme, na pia amewataka kuheshimu haki za wananchi pamoja na usalama wa makazi yao.