У нас вы можете посмотреть бесплатно KAMATI YA KUDUMU BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMEBELEA MRADI WA UJENZI CATC или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Majengo ya Kisasa ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) yaliyopo Banana–Ukonga, jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ya kikazi iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, ambapo wajumbe wa Kamati walipata fursa ya kukagua hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi na kujionea hali ya maendeleo ya ujenzi unaoendelea. Katika ziara hiyo, Kamati ilipongeza jitihada za TCAA katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo na kuisisitiza Mamlaka kuendelea kumsimamia kikamilifu mkandarasi anayetekeleza ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika. Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuwekeza katika sekta ya usafiri wa anga kupitia ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya anga pamoja na kuimarisha mifumo ya usimamizi, akibainisha kuwa rasilimali watu yenye ujuzi wa hali ya juu ni msingi wa ukuaji na usalama wa sekta hiyo. Akizungumza kwa upande wa TCAA, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Salim Msangi alibainisha kuwa CATC ina upekee wa kimkakati kwa kuwa ni miongoni mwa vyuo tisa barani Afrika vinavyotambuliwa katika kutoa mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga, hali inayoliweka Taifa katika nafasi muhimu ya kikanda na kimataifa katika ukuzaji wa utaalamu wa anga. “Mradi huu unaimarisha nafasi ya CATC kama kitovu cha ubora wa mafunzo ya usalama wa anga barani Afrika na ni uwekezaji wa moja kwa moja katika usalama na maendeleo endelevu ya sekta ya usafiri wa anga nchini,” alisema. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006). Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege. Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba