У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI AWESO ATAKA MKANDARASI MRADI WA MTAMBO WA KUTIBU MAJI KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WAZIRI AWESO ATAKA MKANDARASI MRADI WA MTAMBO WA KUTIBU MAJI KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA. Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso amemtaka Mkandarasi wa ujenzi wa mtambo mpya wa kutibu maji wa Mafiga, Manispaa ya Morogoro kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kuwaondolea wananchi wa Halmashauri hiyo changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji. Mhe. Aweso ametoa agizo hilo Januari 19, 2026 wakati wa hafla ya utiaji saini awamu ya kwanza ya mradi huo iliyofanyika katika eneo la Mafiga na kueleza kuwa hakuna haja mradi huo kuchukua miaka miwili wakati fedha tayari zipo. Aidha, amemuagiza Mkandarasi kutoka China kufanya kazi hiyo usiku na mchana ili ikamilike kabla ya miezi 24 iliyotolewa. “...Mkandarasi afanye kazi hii usiku na mchana... na akiongeza vijana mradi utakamilika kwa wakati na wana Morogoro watapata maji safi na uwekezaji utaongezeka,” amesema Mhe. Juma Aweso Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amesema hana shaka na Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi huo kwani amefanya kazi nzuri katika maeneo mengine, huku akiwataka watumishi wa serikali katika sekta hiyo kutimiza wajibu wao ili kuondoa chuki baina ya Serikali na wananchi. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 400 mkoani humo ikiwemo miradi ya MORUWASA na RUWASA, na kuwataka wananchi kutoharibu miundombinu na kutunza vyanzo vya maji kwa vizazi vya sasa na baadae. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, CPA Saisi Kejo amesema mkataba huo unaofungwa leo Januari 19, 2026 ni mkataba mkubwa kuliko mikataba yote iliyowahi kufanyika katika sekta ya maji. Amebainisha kuwa mkataba huo unakwenda kuondoa nakisi iliyokuwepo katika vyanzo vya uzalishaji wa maji ikilinganishwa na mahitaji ya sasa ya Manispaa ya Morogoro na ukikamilika utaongeza lita milioni 54 za ziada. Ameendelea kwa kusema Mkoa wa Morogoro una uwezo wa kuzalisha lita milioni 47 za maji wakati mahitaji ni lita milioni 81, na mradi huu mpya utakazalisha lita milioni 54 na kuwa na jumla ya lita milioni 101 za maji. MWISHO