У нас вы можете посмотреть бесплатно MAKAMU WA RAIS KUWASILI KESHO RUVUMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MAKAMU WA RAIS KUWASILI KESHO FEBRUARI 26 RUVUMA Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emanuel Nchimbi, anatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi tarehe 26 Februari majira ya saa tisa alasiri katika uwanja wa ndege wa Songea, ambapo atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari, RC Ahmed amesema Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha kumbukizi ya miaka 120 ya mashujaa wa vita ya Majimaji kitakachofanyika tarehe 27 Februari kwenye viwanja vya mashujaa, Manispaa ya Songea. Ameeleza kuwa kabla ya maadhimisho hayo, Dkt. Nchimbi atatembelea mnara wa kumbukumbu, kuzindua jengo la wazee wa baraza la mila na desturi, na kuweka upinde na ngao kwa heshima ya mashujaa. Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Ahmed ametoa wito kwa wananchi wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kushiriki mapokezi ya Makamu wa Rais na pia kuhudhuria maadhimisho ya tarehe 27, akisisitiza kuwa tukio hilo ni la kihistoria na ni ishara ya heshima kwa mashujaa waliopigania uhuru wa nchi.