У нас вы можете посмотреть бесплатно #breakingnews или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Takribani watu saba wanadaiwa kuuawa kutokana na vurugu zilitokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu jana nchini Uganda. Mtandao wa Reuters umeeleza kuwa machafuko hayo yaliibuka usiku katika mji wa Butambala, uliopo takriban kilomita 55 kusini-magharibi mwa mji mkuu Kampala. Msemaji wa Polisi wa eneo hilo, Lydia Tumushabe, amesema kuwa kundi la watu wanaosadikika kuwa wafuasi wa upinzani waliokuwa na mapanga, walivamia kituo cha polisi pamoja kisha kituo kupigia kura kilichokuwa jirani. Amesema Polisi iliwadhibi watu hao kwa kuwatawanya.“Vyombo vya usalama vilijibu kwa kujilinda kwa kuwa watu hao walikuwa idadi kubwa. Polisi walifyatua risasi kwa kujilinda,” ameieleza Reuters, akiongeza kuwa watu 25 walikamatwa. Msemaji huyo wa polisi eneo la Butamaba amesema hana taarifa kuhusu tukio jingine lililotokea katika eneo lake licha ya kuwepo taarifa kuwa watu wengine 10 waliuawa kwenye nyumba moja. Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi Uganda imetangaza matokea ya awali yanaonyesha Yoweri Museveni aknaongoza kwa zaidi ya asilimia 75 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi, kwa mujibu wa hesabu zilizokusanywa kutoka asilimia 59 ya vituo vya kupigia kura. Mpinzani wake mkuu, mwanamuziki maarufu Bobi Wine, yuko nyuma kwa takriban asilimia 21, huku kura zilizobaki zikigawanywa miongoni mwa wagombea wengine sita.