У нас вы можете посмотреть бесплатно MTOTO WA MIAKA 14 AZAMA KWENYE MTO MAMBI KIJIJI CHA NDUMBWE MTWARA| JESHI LA ZIMAMOTO LATHIBITISHA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mtoto aitwae Nasri Issa Usi mwenye miaka 14 Mkazi wa Kijiji cha Ndumbwe Halmashauri ya wilaya ya Mtwara amezama kwenye Mto Mambi ulioanzia Kijiji cha Kitere Mtwara na kumwaga Maji yake bahari ya Hindi kwenye Kijiji cha Ndumbwe. Tukio hilo limetokea siku ya Machi 07, 2026 wakati Watoto Wanne akiwemo aliyezama Majini kuanza kubishana walipofika kwenye Mto huo kwa ajili ya kuvua samaki kuwa kina cha Maji ni kifupi ndipo Mtoto huyo alipojaribu kuingia na hiyo ndo ilikuwa mara ya mwisho kuonekana. Watoto waliosalia walirudi nyumbani, walitoa taarifa kwa Wazazi wao ila kwa kuchelewa na ndipo harakati za kumtafuta zilipoanza na mpaka sasa bado hajaonekana. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Ndumbwe Ndg. Ally Mshamu, amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo, ametoa taarifa kwa Viongozi mbalimbali ambao kwa pamoja wameshirikiana kumtafuta bila mafanikio. Nae Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zima moto na uokoaji Mkoa wa Mtwara ASF Ambros Ndunguru, amesema wanaendelea na zoezi la kumtafuta Mtoto huyo ambapo wamefika Mapema baada ya kupokea taarifa hiyo. Hata hivyo Ndunguru ametoa wito kwa Wananchi, kutoa taarifa kwa haraka pale tukio linapotokea, kwa kupiga simu namba 114.