У нас вы можете посмотреть бесплатно KIVUKO CHA MV KILAMBO KUREJEA WIKI IJAYO | KUENDELEA NA SAFARI ZAKE MTWARA - MSUMBIJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wananchi na Wafanyabiashara wa Kijiji cha Kilambo Kata ya Tangazo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, wamehoji ni lini Kivuko cha MV KILAMBO kinachofanya Safari zake Kati ya Tanzania na Msumbiji kupitia boda ya Kilambo kitarejeshwa baada ya kuchukuliwa zaidi ya miaka minne iliyopita na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA kwa ajili ya ukarabati Mkubwa. Wakiongea na Faida Online TV Wananchi hao wamesema Hali ya mzunguko wa Fedha umekuwa mdogo ukilinganisha na wakati ambao Kivuko hicho kilikuwepo na kufanya hali ya Uchumi kushuka hasa kwa Mtu mmoja mmoja kwa kuwa watu wanaovuka ni wachache kutokana na aina ya vivuko wanavyotumika sasa kuwa vidogo na kiusalama sio rafiki ukilinganisha na Kivuko cha MV KILAMBO. Nae Fundi Mkuu wa TEMESA Kanda ya Kusini Bw. Abdurahmani Amir, amesema Kivuko hicho kinatarajia kuletwa wiki ijayo ili kuendelea na Kazi yake katika eneo hilo. Hata hivyo Serikali ipo kwenye mchakato wa kujenga Daraja katika Boda hiyo ya Kilambo, kama ilivyojenga Mtambaswala hali itakayopelekea kukua kwa Uchumi katika Nchi Wanachama wa SADC Tanzania ikiwemo, na Mataifa mengine. SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU.