У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YAKE YA BAJAJI, RC TANGA AKABIDHI KWA MUHUSIKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Tanga amekabidhi bajaji kwa ndugu Shaban Nassoro Sabuni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyopewa wakati wa ziara yake mkoani humo. Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa Mkoa aliendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhimiza falsafa ya kazi na utu iliyowezesha kuwagusa na kuwasaidia wananchi mbalimbali. Alisema kuwa wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika wilaya zote nane za Mkoa wa Tanga, alikagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi, kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Akiwa jijini Tanga, alipata kukutana na ndugu Shaban Nassoro Sabuni, ambaye ni mlemavu wa miguu, na alimweleza changamoto yake ya usafiri ili aweze kujipatia kipato na kulea familia yake. Kwa kuongozwa na dhamira ya kuwasaidia wananchi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba aliagiza fedha zitumike kununua bajaji. Leo bajaji hiyo imempatiwa rasmi ndugu Shaban Nassoro Sabuni. Kwa upande wake, Shaban Nassoro Sabuni amemshukuru Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kutimiza ahadi yake na amesema bajaji hiyo itakuwa msaada mkubwa katika kutafuta kipato na kuboresha maisha yake na ya familia yake. Mkuu wa Mkoa aliwapongeza watumishi wa umma na viongozi wote kuendelea kusikiliza kero za wananchi na kuchukua hatua pale inapowezekana ili kuleta maendeleo endelevu.