У нас вы можете посмотреть бесплатно DARAJA LA ZAMANI LA MTO MARA LASOMBWA NA MAJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Daraja la zamani la mto Mara linalotenganisha Wilaya ya Tarime na Serengeti limesombwa na maji huku nyumba zilizoko jirani zikizingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Leo Alhamisi Aprili 23, 2020 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amefika eneo la tukio na kueleza kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha. Amewataka wananchi kutosogea eneo hilo kwa kuwa maji yanazidi kuongezeka na kwamba kama kusingekuwa na daraja jipya mawasiliano kati ya sehemu hizo yangekatika huku akiwaonya wananchi kutopitisha mifugo katika daraja hilo, kutaka wapakie mifugo kwenye magari. Mwenyekiti wa kitongoji cha mto Mara, Gisiri Mkare amesema wamefanikiwa kuokoa baadhi ya samani za nyumba zilizozingirwa maji. Mmoja wa waliokumbwa na mafuriko, Werema Kisyeri amesema asubuhi alishtuka kuona maji yamejaa ndani, “niliokoa vitu vichache baada ya msaada kutoka kwa majirani.” Peter Bigoti mkazi wa kitongoji hicho amesema alifika nyumbani kwa Werema baada ya kusikia kelele na kumsaidia kuokoa vitu.