У нас вы можете посмотреть бесплатно MIAKA 3 YA MRADI WA "WE CARE " MKOMBOZI KWA WATOTO IRINGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MKOA WA IRINGA Mtazamaji karibu katika Makala hii maalum Hii ni Makala inayokujia kutoka Mkoa wa Iringa, Leo tunaangazia mradi jumuishi wa WE CARE…. Lengo hasa la Makala hii ni kuona matokeo chanya ya mradi unaotekelezwa na mashirika yasiyo ya Kiserikali ya CALL AFRICA, IBO ITALIA na COPE wa kushirikiana na Serikali. Elimu-jumuishi imekuwa ikikuzwa kimataifa kwa miaka mingi, lakini mapungufu makubwa ya takwimu na ushahidi yameathiri upangaji wa miundo na utekelezaji wa sera na mifumo ya elimu-jumuishi. Watoto wenye ulemavu mara nyingi hawaonekani hivyo kupelekea kukosekana uboreshwaji wa fursa zao –za- masomo - na maisha. Utekelezaji wa Mradi huu wa WE CARE ni nyanja muhimu yenye kuleta suluhisho, utekelezaji wa mradi una lengo la kuongeza watoto wenye ulemavu kwenye mfumo wa shule ili waweze kupata fursa ya elimu, miundo mbinu bora na kupata huduma ya utengamao ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoa huduma. Ibo Veneranda Ugi mwenye ulemavu wa kutosikia anasema michezo ni kitu pekee anachokipenda, anawashukuru wadau kupitia shirika la COPE na mradi huu wa WE CARE kuwajumuisha wenye ulemavu. Katika Mradi huu wa WE CARE pia kuna mfumo wa panda, mfumo huu unazingatia siku elfu moja za mtoto Pongezi kwa wadau hawa na Serikali kwa uhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata haki yao ya msingi Kwa mantiki hiyo tunatoa wito kwa jami na Seikali kuendeleza jitihada hizi kwa kuwapa watoto wenye ulemavu fursa sawa na wengine , kuondoa vikwazo vya kimwili, kifedha, na kimiundombinu vinavyowasababishwa wakaachwa nyuma katika jamii. Jina langu ni Tukuswiga Mwaisumbe #wecare #CallAfricaTZ #IBOItalia #COPE @Iringa@