У нас вы можете посмотреть бесплатно MFUMO WA M MAMA ULIVYO OKOA MAISHA YA MTOTO DERICK - MUFINDI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MFUMO WA M MAMA ULIVYO OKOA MAISHA YA MTOTO DERICK - MUFINDI Kila Mama ambaye ni mjamzito anayo haki ya kuwa hai na kuwa salama kabla, wakati na mara baada ya kjifungua Maelfu ya wanawake wajawazito katika maeneo ya vijijini barani Afrika hawawezi kusafiri kwenda hospitalini katika dharura. Hapa ni Wilaya ya Mufindi katika familia ya Bwana na Bibi Mwalongo, wanufaika wa huduma ya M MAMA pamoja na mratibu wa M MAMA hapa Mufindi Huduma hii ya M MAMA hufanyika katika mifumo rahisi ya teknolojia katika kuunganisha wanawake wajawazito au mama na mtoto mchanga kwenye usafiri wa dharura, Huduma hii ni muhimu sana katika maeneo ya vijijini, ambapo hospitali mara nyingi hazipo ama vituo vya afya vipo mbali na mara nyingine kuna changamoto ya miundo mbinu, madereva wanaotumika katika huduma hii ni madereva jamii. Kutana ana na ndugu Butho Jumanne dereva jamii kutoka kata ya Mninga. Uwepo wa madereva na usafiri huu wa kijamii hapa Nchini umesaidia kupugnuza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga na punguzo la gharama kwa kila safari ya dharula Moses Tawete mratibu wa M MAMA Mkoa wa Iringa anasema tangu mwaka 2023 kina mama na watoto zaidi ya elfu 6 wamepatiwa rufaa na kufikiwa na huduma ya M MAMA. Halmashauri hii ya Mufindi ina vijiji 121, Katika utoaji wa huduma za M MAMA katika Halmashauri hii wanatamani vijiji vyote vingeweza kuwa na madereva jamii Dokta Silyvia Mamkwe Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa anazungumzia mwitiko wa wananchi katika kutumia mfumo huu wa MMAMA Serikali ya Tanzania ilianzisha m-mama mwaka wa 2013 kama mpango wa majaribio wa kuratibu usafiri wa haraka, wa kuaminika kwa akina mama walio na uchungu wa uzazi na waliojifungua na watoto wao wachanga katika maeneo ya vijijini. Tanzania ilifikisha huduma nchi kote mwezi Desemba 2023, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliongoza mpango huo, ambao umepunguza vifo wakati wa uzazi kwa asilimia 38 na vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 40. MTAZAMAJI PIGA NAMBA 115 bure KWA dharula ya mama Mjamzito ama mwenye mtoto mchanga. mimi ni Tukuswiga Mwaisumbe