У нас вы можете посмотреть бесплатно BILIONI 78 KUJIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI HANANG' KWA MWAKA 2026/27 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
BILIONI 78 KUJIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI HANANG' KWA MWAKA 2026/27 Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Mkoa wa Manyara, limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 78.94 kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Bajeti hii inakusudia matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24.2 ukilinganisha na bajeti ya sasa ya shilingi bilioni 60.3. Rasimu hiyo imewasilishwa na Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Erick Kayombo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani ulioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. George Bajuta. Kabla ya kupitishwa rasmi, madiwani walipata nafasi ya kuipitia na kuijadili kwa kina, kutoa maoni na mapendekezo ya maboresho ili kuhakikisha bajeti inazingatia vipaumbele vya wananchi na mwelekeo wa maendeleo ya Halmashauri. Miongoni mwa hoja zilizojadiliwa kwa uzito ni pamoja na mbinu zinazotumika katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, kudhibiti upotevu wa mapato hasa yatokanayo na mazao, ukodishaji wa mashamba, na vibanda vya stendi. Aidha, madiwani wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha Halmashauri inapata rasilimali za kutosha kugharamia huduma na miradi ya maendeleo. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Mwalimu Geoffrey Abayo, amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa wataalamu katika kutekeleza majukumu yao kwa mshatakabali wa Hanang'.