У нас вы можете посмотреть бесплатно NMB YALETA TABASAMU HANANG' DC или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
NMB YALETA TABASAMU HANANG' DC Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' imepokea msaada wa vifaa vya elimu na afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 45 kutoka Benki ya NMB, ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha huduma za jamii. Makabidhiano ya msaada huo yamefanyika Februari 3, 2026, katika viunga vya shule ya Sekondari Katesh yakiongozwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang', Mheshimiwa Almishi Isa Hazali, na kuhudhuriwa na viongozi wa Halmashauri, madiwani pamoja na wadau mbalimbali. Mheshimiwa Hazali, ameipongeza Benki ya NMB kwa kuonesha uwajibikaji kwa jamii, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu kwa wananchi. Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 600, madawati 50, vitanda 40 na mabenchi 20 kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya, vifaa vyote vina thamani ya shilingi milioni 45.4 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo, akisema umeongeza nguvu katika jitihada za Halmashauri za kuboresha mazingira ya kujifunzia na utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa George Bajuta, ametoa wito kwa taasisi zingine na wadau wa maendeleo kuiga mfano wa Benki ya NMB kwa kushirikiana na Halmashauri katika kuchangia maendeleo ya elimu, afya na ustawi wa jamii kwa ujumla.