У нас вы можете посмотреть бесплатно WAKULIMA WA HANANG' WANUFAIKA NA MGAO WA MATREKTA 20 YA MKOPO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WAKULIMA WA HANANG' WANUFAIKA NA MGAO WA MATREKTA 20 YA MKOPO Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Almishi Hazali, Jana Oktoba 16, 2025 amewakabidhi wakulima matrekta 20 yaliyotolewa kwa mkopo na kampuni ya KANU Equipments kwa kushirikiana na taasisi ya PASS Leasing. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya amesema hatua hiyo inalenga kukuza matumizi ya zana bora za kilimo na kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika shughuli za kilimo wilayani Hanang akihimiza wakulima kutumia matrekta hayo kwa ufanisi ili kuongeza tija ya uzalishaji na kuchochea maendeleo ya uchumi wa wilaya. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, CPA John Kajivo, amesema halmashauri itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wakulima wanapata fursa za kufanya kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji. Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Daniel Luther, amesema kati ya matrekta 20 yaliyokabidhiwa, 17 yamechukuliwa na wakulima kutoka ndani ya Wilaya ya Hanang, hatua inayothibitisha mwamko mkubwa wa wakulima katika kutumia teknolojia ya kisasa ya kilimo.