У нас вы можете посмотреть бесплатно MADAKTARI BINGWA WA MKOA WATUA HANANG', WANANCHI MJITOKEZE KUPATA HUDUMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MADAKTARI BINGWA WA MKOA WATUA HANANG', WANANCHI MJITOKEZE KUPATA HUDUMA Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo amezindua rasmi Kambi Maalumu ya Madaktari Bingwa wa ndani ya mkoa huo katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang, Tumaini. Mheshimiwa Sendiga ameeleza kuwa, kambi hiyo ni utekelezaji wa Programu ya Madaktari Bingwa wa ndani ya Mkoa wa Manyara, ambapo kila halmashauri inatenga bajeti ya ndani kuwaleta madaktari bingwa ili kusogeza huduma karibu na wananchi ambapo halmashauri ya Wilaya ya Hanang' ni ya tatu kutekeleza mpango huu. Akitoa taarifa ya kambi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hanang', Dokta Mohammed Kodi, amesema mpango huu unalenga kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi na kuwapunguzia gharama za matibabu. Kwa mujibu wa Dkt. Kodi, kambi hiyo ilianza jana na tayari wananchi 300 wamepata huduma malengo ikiwa ni kutoa huduma za kibingwa kwa zaidi ya wananchi 1,500 kutoka wilayani Hanang na maeneo ya jirani kwa muda wa siku tano. Huduma za kibingwa zinazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na; Upasuaji, Matibabu ya magonjwa ya ndani (moyo, kisukari na shinikizo la damu), Huduma za afya ya wanawake na uzazi, Matibabu ya watoto, Huduma za macho pamoja na Huduma za masikio, pua, koo na usikivu