У нас вы можете посмотреть бесплатно WIZARA YA KILIMO YAZINDUA JUKWAA LA WADAU MRADI WA FOLUR KASKAZINI UNGUJA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Katika juhudi za kuthamini mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Wizara ya Kilimo Zanzibar leo imezindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Mradi wa FOLUR katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa lengo la kurejesha na kuboresha mandhari ya misitu. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini ‘B’ Unguja, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’1, Ndugu Juma Sururu Juma, amesema mradi huo ni chachu muhimu ya kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika mkoa huo. Amewataka masheha na viongozi wa maeneo mbalimbali kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio na kuleta matokeo chanya kwa jamii. Ameongeza kuwa uongozi wa mkoa na wilaya uko tayari kuunga mkono jitihada hizo huku akiwahimiza wadau kujikita katika kutatua changamoto zitakazojitokeza ili mradi huo uwe nyenzo ya kuimarisha maendeleo endelevu ndani ya visiwa vya Zanzibar na Pemba. Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa FOLUR Zanzibar, Ndugu Miza Suleiman Khamis, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kutekeleza mradi huo kwa lengo kuu la kurejesha uoto wa misitu na kuhakikisha mazingira yanakuwa himilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi. Naye Mratibu kutoka Tanzania Bara, Joseph Mgana, amesema lengo la kuwakutanisha wadau wa ngazi mbalimbali ni kujadili na kuratibu kwa pamoja masuala ya maendeleo, hususan katika utekelezaji wa miradi inayohusu Mkoa wa Kaskazini Unguja. #FOLUR #Mazingira #MabadilikoYaTabiaNchi #Kilimo #Zanzibar