У нас вы можете посмотреть бесплатно KAMISHENI YA MAAFA ZANZIBAR YAENDESHA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar imeandaa mafunzo ya siku mbili kwa kushirikiana na United Nations Development Programme (UNDP) yanayolenga kujenga uwezo kwa wakuu wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Mafunzo hayo yamekusudia kuongeza uelewa na kuimarisha mikakati ya maandalizi, kinga na mwitikio dhidi ya athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo mafuriko, ukame na mabadiliko ya mifumo ya mvua. Washiriki wameeleza kuwa mafunzo hayo yataongeza chachu ya ufanisi katika taasisi zao kwa kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza, pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi. Aidha, imeelezwa kuwa suala la mabadiliko ya tabia nchi si jukumu la Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa pekee, bali linahitaji ushiriki wa kila taasisi na mwananchi kwa ujumla ili kupunguza athari na kujenga ustahimilivu wa jamii. #MabadilikoYaTabiaNchi #Maafa #Zanzibar #UNDP #Maendeleo