У нас вы можете посмотреть бесплатно Fafanuzi rahisi ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana - Mapigo Ya Baragumu Sura ya 8 na 9 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Fafanuzi rahisi ya kitabu cha Ufunuo wa Yohana - Mapigo Ya Baragumu Sura ya 8 na 9 Mapigo ya baragumu sita za mwanzo – Sura ya 8 na ya 9 Tuliangalia hapo juu, kwamba 8:1-5, hutaja habari za pigo la Muhuri ya Saba, wakati Mungu anajibu maombi ya watakatifu waliochinjwa kwa ajili ya ushuhuda wa Neno la Mungu, maombi yaliyoombwa wakati wa muhuri ya Tano (6:9-11). Sasa, yanayofuata ni mapigo ya Baragumu saba. Mapigo yote haya yatawapata wanadamu waliokataa kumwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Baragumu ya Kwanza: Kutatokea mvua ya mawe na moto vilivyochangamana na damu 8:7. Pigo hili linafanana na pigo la saba juu ya Misri wakati wa Musa – Kutoka 9:18, 22-25. Baragumu ya Pili: Theluthi ya bahari itageuzwa kuwa damu 8:8,9. Pigo hili lilikuwa ni pigo la kwanza la Musa juu ya Misri – Kutoka 7:20,21. “Aligeuza damu mito yao. Na vijito wasipate kunywa” ZABURI 78:44 Baragumu ya Tatu: Theluthi ya maji yatakuwa machungu 8:10,11. “13 Naye Bwana asema, Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu niliyoweka mbele yao, wala hawakuitii sauti yangu, wala kuenenda katika hiyo; 14 bali wameenenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe; na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao. 15 Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe.” Yeremia 9:13-15. Baragumu ya Nne: Theluthi ya jua, mwezi na nyota kupigwa ili pawepo giza 8:12. Hilo lilikuwa pigo la tisa katika Misri. Kutoka 10:21-23. Baragumu ya Tano: Inatolewa ‘Ole’, ndipo mapepo mfano wa nzige watatokea juu ya nchi 9:1-12. Pigo kama hili lilikuwa ni pigo la nane juu ya Misri – KUTOKA 10:12-15. Hawa nzige katika baragumu hii ya tano, si nzige wa kawaida, bali ni mapepo. Kwa sababu:- i. Watatoka katika moshi wa kuzimu, ni viumbe wa kutoka kuzimu; hawatadhuriwa na moto wala moshi 9:3. ii. Hawatakula majani, nzige wa kawaida hula majani 9:4. iii. Watawatesa wanadamu, kinyume cha nzige wa kawaida 9:5,6. iv. Nzige hawa wana mfalme 9:11. Tunasoma katika Mithali 30:27 kwamba nzige wa kawaida hawana mfalme. Baragumu ya Sita: Itatolewa ‘Ole’ ya pili, ndipo malaika wanne wa ghadhabu watafunguliwa, nao wanakuja na watu wa ajabu kutoka kuzimu. Idadi ya watu wapatao milioni mia mbili (200,000,000) - 9:13-21. Baragumu ya Saba: Inatajwa katika sura ya 11:15-19, wakati wa kipindi cha Pili cha Dhiki Kuu. #ufunuowayohana #bishop #fredricksimon