У нас вы можете посмотреть бесплатно VETA GEITA TUMAINI JIPYA GEITA , DC AAGIZA VIJANA WAPEWE KAZI TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Taasisi za serikali na zile za binafsi wilayani Geita zimetakiwa kuwapa kipaumbele vijana waliohitimu mafunzo ya Ufundi Stadi kupitia VETA Mkoa wa Geita kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kupunguza wimbi la changamoto ya ajira linalowakabili vijana nchini. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ufundi Stadi VETA Manispaa ya Geita ambapo amesema miradi mingi inayotekelezwa katika Halmashauri na taasisi nyingine imekuwa ikihitaji mafundi wenye ujuzi wa kati, hivyo kuwajumuisha wahitimu wa VETA kutasaidia si tu kupunguza ukosefu wa ajira, bali pia kuboresha ubora wa kazi. Mkuu wa chuo hicho Tadeus Panga amesema Kwasasa chuo hicho kinatoa kozi tano na kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi zaidi ya 900 kwa kozi fupi na 520 kwa kozi ndefu nakwamba Fani zilizopo kwasasa ni Ufundi Bomba , Umeme wa Majumbani, Uhazili na Kompyuta , upishi na umeme wa magari huku akieleza changamoto zilizopo.