У нас вы можете посмотреть бесплатно SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA KUZIMA MOTO IRINGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali mkoani Iringa imejipanga kushughulikia majanga ya moto kwa ufanisi zaidi ili kuokoa maisha ya wananchi na mali zao, kufuatia hatua ya kuimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vifaa na magari mapya ya kisasa. Akizungumza leo wakati wa hafla ya kukabidhi magari sita ya kuzimia moto kwa awamu ya kwanza, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, alisema mkoa wa Iringa ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kubwa na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi. “Serikali imeamua kuwekeza katika vifaa vya kisasa ili kuhakikisha tunakuwa tayari kukabiliana na majanga kwa wakati. Tunataka wananchi waishi kwa usalama na shughuli za kiuchumi ziendelee bila hofu,” alisema Kheri. Kwa upande wake, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Iringa, Jackline Mtei, alisema ujio wa magari na vifaa hivyo utarahisisha kazi ya kuzima moto kwa ufanisi zaidi, kwani vina uwezo mkubwa wa kufikia maeneo mbalimbali kwa haraka. “Awali tulikuwa tunakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa, lakini sasa tuna imani tutaongeza kasi ya majibu ya dharura,” alisema Mtei. Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo waliipongeza serikali kwa kuimarisha huduma za zimamoto, wakisema hatua hiyo itasaidia kupunguza madhara yanayosababishwa na majanga ya moto. Waliahidi pia kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa sahihi pindi ajali ya moto inapojitokeza.