У нас вы можете посмотреть бесплатно MBUNGE MWAMENGO ALIVYOWAKOSHA IPINDA MAJIBU UTATUZI WA KERO ZAO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
JANA siku ya Jumatano, Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mheshimiwa Baraka Ulimboka Mwamengo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Ipinda na jirani, ukiwa na lengo la kushukuru kwakumchagua, kutoa mrejesho wa utekelezaji alioufanya pamoja na kusikiliza kero za wananchi. Wananchi wa Ipinda wameshukuru kwa kufikiwa na mkutano huo, ikiwa ni jambo ambalo halikuwepo hapo mwanzo. Pamoja na hilo, wametoa changamoto zao haswa upande wa maji, elimu, afya, bei ya zao la kakao na miundombinu ya usafiri. Hata hivyo, Mheshimiwa Mwamengo aliwakosha wananchi hao kwa namna alivyojipanga kuleta majibu ya utekelezaji wa kero zao. Mwamengo aliambatana na wataalamu wa kila sekta, ambapo walitolea majibu ambayo yaliwakosha wananchi hao huku wakiwa na matarajio ya utekelezaji wake. Kwa upande wake, Mwamengo ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizowasilishwa. Amesema, kwazile zilizo ndani ya uwezo wake anaahidi atazitekeleza kwa wakati, huku akiwataka wampe subira kwa changamoto zinazohitaji Serikali kuu. Amesema atahakikisha ataendelea kuziwasilisha Serikali kuu na Bungeni kwenye bunge la bajeti lijalo. "Kwa upande wa bei ya kokoa, hapa Naomba tuambiane ukweli. Tatizo lililopo ni kushuka Kwa bei ya soko la dunia, ndio maana mtaona hata hapa nchini, kote Morogoro, Busokelo bei imeshuka" Amesema Mwamengo. Hata hivyo amewaahidi wananchi kuhakikisha anafuatilia ahadi ya Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan, ambayo aliitoa ya kuhakikisha anafanikisha usindikaji wa kakao hapahapa nchini, ili kulipa thamani kubwa zoa hilo.