У нас вы можете посмотреть бесплатно OPERESHENI YA KUSHTUKIZA YABAINI UTAPELI WA AJIRA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#HABARI: Vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Tabora vimefanya operesheni ya kushtukiza na kufumania mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini waliokuwa wamekusanywa katika vituo vitatu kwenye kata za Mpela na Mtendeni kwa madai ya kupewa ajira na fursa za kibiashara. Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Bi. Upendo Wella, amebainisha kuwa vijana hao walirubuniwa na kutozwa hadi shilingi milioni nne kila mmoja kwa sharti la kuuza bidhaa za biashara mtandao ili kupata bonasi, jambo lililopelekea Serikali kusitisha shughuli hizo mara moja ili kudhibiti utapeli huo. Katika operesheni hiyo, Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Shani Mdamu, ameonya juu ya hatari ya vijana hao kujihusisha na uuzaji wa bidhaa za afya bila kuwa na taaluma yoyote, huku baadhi ya vijana wakieleza jinsi walivyoshawishiwa kuingia katika mfumo huo. Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ametoa maamuzi ya Serikali ya kufunga vituo hivyo, huku msimamizi wa kimoja cha vituo hivyo, Bw. Saitoti Lekando, akipokea agizo hilo la kusitishwa kwa shughuli zao zilizokuwa zikiwaumiza vijana kiuchumi. Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania #Follow @itvtz @radioonetanzania @capitaldigitaltanzania Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3 Twitter : https://bit.ly/2XG7aii Instagram : https://bit.ly/34KItmg