У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 15/01/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 15/01/2026 UJUMBE WA LEO: UNAFANYAJE KUNAPOKUWA NA TESO LA KUJIRUDIA RUDIA KWENYE LANGO LA FAMILIA (MLIVYOZUNGUKA MLIMA HUU VYATOSHA) 3) Watu Wenye Ndoto Kubwa na Maono ya Mbali. Ayubu 38 : 12 - 13 12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake? 3 Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo? Zaburi 78:6 Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao Waamuzi 11 : 1 - 3 1 Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. 2 Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine. 3 Ndipo Yeftha akawakimbia hao nduguze, akakaa katika nchi ya Tobu; na watu mabaradhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye. Nehemia 1 : 1 - 4 1 Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni, 2 Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliopona, hao watu wa uhamisho waliosalia; na habari za Yerusalemu. 3 Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. 4 Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni; Hawa ni watu wanaotamani kuvuka mipaka ya familia, mazingira, na historia ya ukoo. Kwa nini hukutana na vizuizi? Ni neema iliyo juu yao ya kuona vitu kwa mtazamo tofauti na kupambana kuleta mabadiliko, Huwa wanasumbuka sana na hali ilivyo kwenye Familia, kwenye ukoo kwenye taasisi wakati wengine wanaona ni jambo la kawaida. Watu ambao kila Mwaka wanawaza kujenga Kuta za Familia, ukoo, taasisi zilizovunjika kila ukisikia habari ya kwenu inakuumiza na kukutesa wakati wengine wanapokea kawaida, Mipaka ya familia inapambana nao. Ndio Watu ambao tutaambiwa amesoma sana Mpaka wamechanganyikiwa Vita ya miungu inayovuruga alichobeba. Ndio watu ambao wanapoteza focus kwa haraka na hatujui nini kimewapata! Wanabeba Uchungu na maumivu kiasi cha kupoteza uelekeo. Vita haviendi kwa wepesi kwenye maisha yao. KWA NINI ADUI ANANYANYUA VITA JUU YAO? Kuuwa Maono na Mipango ya kivizazi. Shetani hana shida na kazi matokeo na baraka yoyote isiyo na mwendelezo wa kivizazi. 2 Samweli 7 : 12 - 16 12 Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. 13 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. 14 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu; 15 lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako. 16 Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele. VITA YA UZAO INAYOVURUGA UWEZO 1. Kuwaondoa wanao kwenye kweli ya Mungu ili ukose mrithi wa vitu vya Ki-Mungu ulivyobeba. (Mjue sana Mungu ili uwe na Amani ndivyo mema yatakujilia). Mwanzo 18 : 17 - 19 17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, 18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? 19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Vita nyingine ya Msimu mpya ni vita ya adui kugusa Uzao wako ili kuvuruga ulichobeba. Waamuzi 2 : 8, 10 8 Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi. 10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. Mhubiri: Mwl.James Kamera Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com