У нас вы можете посмотреть бесплатно MOROGORO NA UTAJIRI WA KILIMO CHA KUWAINUA WANANCHI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MOROGORO NA UTAJIRI WA KILIMO CHA KUWAINUA WANANCHI. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amesema ajenda ya maendeleo katika mkoa huo imejikita katika sekta ya kilimo cha mazao ya kimkakati, hatua itakayoinua vipato vya wakulima na mkoa kwa ujumla. Hayo ameyabainisha Februari 16, 2026, mkoani Morogoro wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichoketi kujadili na kutathmini bajeti ya mkoa, ikiwa ni hatua ya awali katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Mkuu wa Mkoa Adam Malima amesema kuwa mkoa umeweka mikakati madhubuti ya kuinua vipato vya wananchi kwa kukuza sekta ya kilimo cha mazao ya kimkakati likiwemo zao la korosho, karafuu, kokoa, parachichi na michikichi. “Tunataka kujenga Morogoro ambayo itakuwa mkoa tajiri kwa kipato kwa kila mwananchi kinachotokana na kilimo kuliko mkoa wowote nchini Tanzania,” amesisitiza Adam Malima. Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa katika sekta ya ufugaji, mkoa umejipanga kuhakikisha wafugaji wanatumia njia za kisasa za ufugaji, hususan unenepeshaji wa mifugo, jambo litakaloongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo. Mwisho.