У нас вы можете посмотреть бесплатно Tanzania kujitosheleza kwa sukari. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tanzania kujitosheleza kwa sukari. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha suala la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi linakuwa historia, kufuatia uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa katika sekta ya uzalishaji wa sukari nchini ambayo inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Prof. Mkumbo ametoa kauli hiyo Februari 25, 2026, wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Morogoro alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mkoani humo. Amesema, umefika wakati kwa Tanzania kujitegemea katika uzalishaji wa sukari na bidhaa nyingine ili kuimarisha uchumi wa taifa na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha uwekezaji kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayovutia wawekezaji zaidi na kuongeza tija ya uzalishaji viwandani. Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo amesema Wizara ya Kilimo itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Mipango na Uwekezaji ili kuhakikisha uwekezaji unaofanyika nchini unaleta tija halisi kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Prof. Mkumbo amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejipanga kuimarisha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, lengoni kujitosheleza kwa chakula ikiwemo sukari kama sehemu ya mkakati huo, amebainisha kuwa ushirikiano kati ya wizara hizo mbili utasaidia kuvutia uwekezaji, kuongeza ajira na kuimarisha mchango wa sekta ya kilimo katika pato la taifa. Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima amesema, jitihada za Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kujitosheleza katika uzalishaji wa sukari zimeanza muda mrefu na kwamba Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kimekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uwekezaji na kuimarisha uchumi wa mkoa huo. Aidha amesema Serikali ya Mkoa huo haitamvumilia mtu yeyote kuhujumu au kuleta mzaha katika masuala ya uwekezaji, hususan uvamizi wa mifugo katika mashamba ya miwa, jambo linaloathiri uzalishaji na kusababisha hasara kwa wawekezaji huku akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachobainika kuvamia mashamba ya wawekezaji mkoani humo. Mwisho.