У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MALIMA AAGIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RC MALIMA AAGIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amewaagiza wenyeviti wa halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utunzaji, usimamizi na uhifadhi wa vyanzo vya maji, huku akisisitiza kuwa suala hilo ni la kipaumbele katika maendeleo ya mkoa huo. Malima ametoa agizo hilo Februari 16, 2026, mkoani Morogoro wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika ukumbi wa Magadu Manispaa ya Morogoro ili kujadili na kutathmini bajeti ya mkoa, ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Katika kikao hicho, Malima amesisitiza kuwa umefika wakati wa kuchukua hatua madhubuti za kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali hiyo ya majiunakuwepo kwa kuwa una umuhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. “Naomba wenyeviti wa halmashauri mtusaidie sana. Uchafuzi wa mazingira unazidi kwa kasi kubwa sana. Jitihada za kutunza mazingira ni wajibu wa kila Mwanamorogoro,” amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa. Aidha, Kiongozi huyo wa juu kabisa katika Serikali ngazi ya Mkoa amezielekeza halmashauri zote za Mkoa huo kuweka mikakati ya kuvutia wawekezaji utakaosaidia maendeleo ya mkoa na kunufaisha moja kwa moja wananchi mmoja mmoja na taifa. Kwa upande wa Sekta ya Afya, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Best Magoma, ameeleza suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ndani ya mkoa huo kuwa ni 83%. Ongezeko hilo limetokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali, jambo lililosababisha malalamiko ya wananchi kupungua kutokana na kupata huduma ambazo awali hawakuwa wakizipata ndqni ya mkoa. Naye Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Bi. Sarah Msafiri, ameshauri kuwa mpango wa maendeleo wa Dira ya Taifa ya mwaka 2050 unachangiwa na sekta binafsi. Hivyo, kama viongozi wa mkoa, wana wajibu wa kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kukuza sekta ya kilimo na ufugaji. Mwisho.