У нас вы можете посмотреть бесплатно MASHINDANO YA KUHIFADHISHA QUR’AN YATAJWA KUJENGA MAADILI KWA VIJANA KWAHANI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Mhe. Hamza Hassan Juma, amesema mashindano ya kuhifadhisha Qur’an yana mchango mkubwa katika kujenga maadili mema kwa jamii ya Kiislamu, hasa katika kipindi hiki cha mwingiliano mkubwa wa tamaduni. Ameyasema hayo katika mashindano ya kuhifadhisha Qur’an yaliyoandaliwa na viongozi wa Jimbo la Kwahani, yaliyofanyika Skuli ya Muungano Kibanda Maiti, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amefafanua kuwa mashindano hayo huwasaidia watoto na vijana kuelekezwa katika misingi sahihi ya dini, hatua inayowalinda dhidi ya mmomonyoko wa maadili na mienendo isiyofaa katika jamii. Aidha, ameupongeza uongozi wa Jimbo la Kwahani kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi walizotoa kwa wananchi, akibainisha kuwa mashindano hayo ni miongoni mwa ahadi hizo. Mhe. Hamza ametoa wito kwa viongozi kuwasikiliza wananchi, huku akiwahimiza wazazi na walimu kuendelea kusimamia malezi na elimu ya watoto ili wakue katika maadili mema na taaluma bora. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Mohd Abdullah Makame Laki, amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao na wazazi kuendelea kuwekeza katika elimu kwa mustakabali bora wa watoto wao. Mashindano hayo, yaliyofanyika kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo, yalihusisha hifadhi ya juzuu ya kwanza hadi ya tano, yakishirikisha vyuo 24 kati ya 50 vya jimbo hilo na jumla ya wanafunzi 36. Washindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tano walikabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo mashine za kushonea, jokofu, jiko la umeme, jiko la kupikia wali pamoja na fedha taslimu.