У нас вы можете посмотреть бесплатно ZAIDI YA WAJANE 360 WAFIKIWA NA IFTARI CHUMBUNI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kutimiza nguzo ya nne ya Uislamu kwa kufanya ibada ya swaumu kwa moyo mkunjufu ili kufikia malengo ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa iftari kwa wajane iliyofanyika katika Skuli ya Dkt. Salmin Amour, Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Ussi Salum Pondeza, amesema zoezi hilo ni sehemu ya kuwafariji na kuwasaidia wajane ili waweze kutekeleza ibada ya swaumu kwa utulivu. Amesema jumla ya wajane 360 kutoka shehia zote za Jimbo la Chumbuni wamefikiwa na msaada huo, ikiwa ni hatua ya kuimarisha mshikamano na kusaidiana katika mwezi huu mtukufu. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni, Makame Mohammed Sufiani, amesema wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha makundi maalum yanapatiwa msaada, hasa katika kipindi cha Ramadhani ambacho mahitaji huongezeka. Nao baadhi ya wajane waliopokea msaada huo, akiwemo Maryam Nassor Mwinyi na Asiya Seif Khamis, wameishukuru Ofisi ya Mbunge na Mwakilishi kwa kuwajali na kuwakumbuka, wakisema msaada huo umewapa faraja na matumaini katika maisha yao ya kila siku.