У нас вы можете посмотреть бесплатно KIKOHOZI/KUKOHOA: Kujitibu mwenyewe nyumbani или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DR.MNIKO #MNIKO #DRMNIKO Kukohoa ni moja ya njia bora sana ya mwili kujilinda. Ukikohoa inasaidia kusafisha kabisa njia ya hewa. Moshi, vumbi au hata ukipaliwa na chakula inaweza kusababisha ukakohoa. Unapokuwa na mafua, makamasi kutoka puani yanaweza kutirirka na kuingia kwenye njia ya hewa na hivyo kusababisha ukohoe. Unaweza kutibu kikohozi hiki kwa kutumia dawa za kikohozi (cough suppressants). Kama mapafu yako yameathirika, ukikohoa itasaidia kutoa makohozi na usaha. Aina hii ya kikohozi ambacho kina makohozi, kinasaidia kusafisha mapafu. Kama kikohozi chako kinatoa makohozi, haipaswi kunywa dawa za kuzuia makohozi (cough suppressants). Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayosababisha kikohozi kwa watu wengi: • Kuvuta sigara kunaua seli zilizo kwenye utando wa njia ya hewa, kwa sababu hii, mwili unashindwa kutoa nje makohozi kwa njia ya kawaida. Mtu anayevuta sigara, anakuwa na kakikohozi kasikoisha • Maambukizi ya virusi yanaweza kusababisha upate kikohozi ambacho kinasababisha utoe makohozi yenye rangi ya njano au meupe. Ukitumia dawa za antibiotiki kwa mtu mweny virusi, hazisaidii, kwa hiyo usijisumbue. Mara nyingi, ukisubiri tu, utapona bila hata kutumia dawa yoyote. • Maambukizi ya bakteria yanaweza kusababisha kikohozi chenye makohozi yenye rangi ya kutu au rangi ya kijani. Kwa kwa kawaida ukiangalia makohozi yake, yanaonekana kama ndani ya ausaha. Aina hii ya kikohozi, daktari atakuandikia dawa ya antibiotiki ili kukutibu. Madaktari mara nyingi watatumia neno “pneumonia” kuelezea ugonjwa wako, usiwe na wasiwasi, neno hili linamaanisha kuwa una maambukizi kwenye mapafu. Kwa watoto wachanga, kukohoa si jambo la kawida, kwa hiyo kama anakohoa mpeleke kwa daktari amkague mapafu yake. Kwa watoto wakubwa, huwa wana tabia ya kumezameza vitu na vinaweza kukwama kooni. Kwa hiyo kuwa makini. Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama una kikohozi Jifukize, unaweza kuchukua bakuli lenye maji ya moto, inamia karibu na bakuli kisha jifunike kitambaa kichwani ili kuvuta mvuke wake au unaweza kuoga maji ya moto, hii pia itasiaida. Kunywa maji ya kutosha itasaida pia hali yako kuwa sawa zaidi. Chagua dawa sahihi kulingana na kikohozi ulichonacho, kama kikohozi chako ni kikavu (hakitoi makohozi) unaweza kutumia dawa za kutuliza kikohozi, ila kama kikohozi kinatoa makohozi usitumie dawa za kuzuia usikohoe, badala yake tumia dawa za kusaidia makohozi yatoke ili upone haraka. Mfano wa dawa utazokuna nazo ni kama ifuatavyo • Zipo dawa zinazosaidia makohozi kutoka (expectorant), mara nyingi zinakuwa na kiambata kinachoitwa guaifenesin, dawa hizi ukienda duka la dawa baridi unazipata bila cheti cha daktari, zinasaidia kulainisha makohozi na kupunguza ukali wa kikohozi. • Zipo pia dawa za kumumunya “cough lozenges” zinasaidia pia kupooza kikohozi kikavu au kikohozi kinachosababisha uwashwewashwe kooni. • Zipo dawa pia zenye kiambata “Dextromethorphan”, hizi zinasaidia kutuliza kikohozi kikavu, hiki ni kile kikohozi ambacho unakohoa na hakuna makohozi yanatoka. Dawa za aina hii utazipata pia madukani. Kama pia una mafua, anaweza kutumia dawa kama “decomgenstants au antihistamines” kama tulivyojifunza wakati tunzungumzia makamasi. SUBSCRIBE