У нас вы можете посмотреть бесплатно NDARO LUBUNDA: PMCU YALETA NEEMA KWA WAKULIMA WA PAMBA, YAWEKA MIKAKATI MADHUBUTI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Pamba Mara (PMCU), Ndaro Lubunda, amesema chama hicho kinaendelea kuleta manufaa makubwa kwa wanachama wake ambao ni wakulima wa pamba kupitia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, huduma za ugani, pamoja na uhakika wa soko la mazao yao. Akizungumza na Mazingira FM mara baada ya kukamilika kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika leo 27 Feb 2026 katika ukumbi wa Mwembeni Complex, Musoma mjini, Lubunda amesema chama kimeweka mikakati madhubuti ya kushughulikia changamoto zinazowakabili wakulima ikiwemo upatikanaji wa pembejeo bora, mitaji, vitendea kazi na changamoto za bei. Ameeleza kuwa kupitia usimamizi imara wa bodi na uongozi wa chama, (PMCU) inaendelea kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la pamba ili kuongeza tija na mapato kwa wakulima, huku akiwahimiza wanachama kuendelea kuwa na umoja na kuamini chama chao kwa maendeleo ya pamoja.