У нас вы можете посмотреть бесплатно DAWA ZA TIBA KUGEUZWA KUWA ZA KULEVYA, MAMLAKA ZASHITUKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DAWA ZA TIBA KUGEUZWA KUWA ZA KULEVYA, MAMLAKA ZASHITUKA Imeelezwa kuwa kutokana na uwepo wa matumizi ya dawa kiholela, licha ya kusababisha usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa za antibiotiki, pia matumizi hayo yamekuwa tatizo linalotokana na watumiaji kuzitumia vibaya dawa zenye viambata vya dawa za kulevya. Hali hiyo imeziibua Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Ziwa kukemea ununuzi wa dawa kiholela unaosababisha baadhi ya watu kuzitumia kama mbadala wa dawa za kulevya. Akizungumza na wakaguzi wa dawa mkoani Mwanza, Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa, Aggrey Muhabuki, amesema kumeibuka kundi la watu wanaotumia dawa za tiba zenye viambata vya dawa za kulevya kiholela mitaani, hali inayosababisha ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya. Muhabuki amewataka wauzaji wa dawa katika maduka maalum kuacha kuuza dawa hizo kwa mtu yeyote bila kuwa na cheti cha daktari au sababu maalum, ili kuepusha matumizi holela ya dawa hizo. Kwa upande wake, Jafari Mtepa, Afisa wa Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Ziwa, amesema sababu nyingine inayowafanya baadhi ya watu kutumia dawa hizo ni kukazwa kwa udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya nchini. Kutokana na hali hiyo, baadhi yao wamegundua mbadala wa kutumia dawa za matibabu. Aidha, amewatahadharisha wauzaji wa dawa katika maduka maalum kuacha kuuza dawa zenye viambata vya dawa za kulevya bila kuwa na sababu maalum au cheti cha daktari kwa mhusika.