У нас вы можете посмотреть бесплатно Swahili: Njia Mbadala za Magari Yanayotumia Petroli | Alternatives to Gas Fueled Cars или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Alternatives to Gas Fueled Cars Njia Mbadala za Magari Yanayotumia Petroli Namna tunavyosafiri inaendelea ikibadilika siku hizi. Watu wengi zaidi wanatafuta njia bora za kufika wanapohitaji kwenda—njia zinazogharimu kiasi kidogo, zinazopunguza uchafuzi wa mazingira, na zinazochangia afya ya jamii zetu. Hebu tuangalie baadhi ya njia mbadala za magari yanayotumia petroli, na jinsi magari hayo yanaweza kuingiliana katika maisha yako ya kila siku. Sekta ya usafiri ni mojawapo ya vyanzo vikubwa vya uchafuzi wa mazingira. Kila tunapoendesha gari la petroli, gesi ya kaboni dioksidi na hewa nyingine chafuzi hutolewa angani. Lakini kuna chaguo safi zaidi—kama magari ya umeme, magari mseto, baiskeli za umeme, na usafiri wa umma kama mabasi na gari la moshi. Chaguo hizi hutumia nishati safi zaidi na hupunguza madhara kwa mazingira. Hata kubadilisha safari moja tu kwa siku kunaweza kuleta tofauti kubwa—kwa hewa tunayovuta na kwa dunia tunayoshirikiana kuishi pamoja. Kwa hivi leo, una chaguo nyingi zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Kuna magari ya umeme (EV), magari mseto yanayo chajiwa, magari mseto ya kawaida, baiskeli za umeme, pamoja na usafiri wa umma. Hakuna chaguo moja linalofaa kila mtu. Lakini kwa pamoja, chaguo hizi zinatupeleka kwenye mfumo wa usafiri ulio safi na wa busara zaidi. Magari ya umeme hutumia umeme pekee yake. Hayatoi moshi kabisa. Ni tulivu, ni kimya, na yana ufanisi mkubwa. Hayana tanki la mafuta wala bomba la moshi. Pia yana vipuri vichache vinavyosogea—hivyo huhitaji matengenezo machache, na hakuna kubadilisha mafuta ya injini. Magari mengi ya umeme yanaweza kusafiri kati ya maili 200 hadi 300 kwa chaji moja kamili. Na vituo vya kuchaji vinaongezeka kila siku. Unaweza kuchaji gari lako nyumbani usiku kucha, na kuanza asubuhi ukiwa na betri iliyojaa. Kama bado hujawa tayari kuhamia matumizi ya umeme pekee, magari mseto ni hatua nzuri ya mpito. Magari mseto ya kawaida hutumia mfumo wa petroli na umeme kwa pamoja ili kupunguza matumizi ya mafuta. Hayahitaji kuchajiwa. Magari mseto yanayo chajiwa hutumia umeme kwa safari fupi,na hubadilika yenyewe kutumia petroli kwa safari ndefu. Yameundwa kujiendesha kwa ufanisi wa juu bila wewe kugundua mabadiliko. Magari haya ni rahisi kubadilika, ya kuaminika, na yanafaa kwa familia zinazoshirikiana matumizi ya gari au kusafiri umbali tofauti tofauti. Lakini kuendesha gari si njia pekee ya kusafiri. Usafiri wa umma ni mojawapo ya njia zenye ufanisi mkubwa wa nishati. Ukiangalia, Mabasi na gari la moshi, adhi zao zikiwa za umeme au mseto—hubeba watu wengi kwa kutumia nishati kidogo zaidi. Hupunguza msongamano wa magari barabarani na hupunguza uchakavu wa barabara zetu. Basi lililojaa linaweza kuondoa magari mengi barabarani. Hii inapunguza hewa chafuzi, inapunguza msongamano, na inalinda miundombinu yetu. Kwa kutumia programu za simu zinazokuonyesha muda wa kuwasili kwa basi au treni, usafiri wa umma unaweza kuwa njia rahisi, ya kuaminika, na ya gharama nafuu. Baiskeli za umeme ni baiskeli zenye mota ya umeme inayokusaidia unapoikanyaga. Ni bora kwa safari fupi na shughuli ndogo ndogo. Ni za haraka, nafuu, na zina nguvu hata kwenye milima. E-bike inaweza kuchukua nafasi ya safari nyingi za gari—na mara nyingi kukufikisha haraka zaidi. Ni mazoezi mazuri kwa mwili, ni nafuu, na ni ya kufurahisha. Kwa muda mrefu, usafiri safi huwa nafuu zaidi. Kuchaji kwa umeme kunaweza kugharimu sawa na kulipa takribani dola moja kwa galoni ya mafuta. Magari ya umeme na mseto huhitaji matengenezo machache— hakuna kubadilisha mafuta ya injini, na vipuri ni vichache. Baiskeli za umeme hugharimu senti chache tu kuchaji. Na tiketi ya mwezi ya basi inaweza kukuokoa mamia za dola ukilinganisha na gharama za kumiliki gari. Kuna uwezekano wa familia yako kustahili kupata fedha za kurejeshewa baada ya kununua—zinazojulikana kama rebate—kutoka kwa kampuni za umeme au serikali za mitaa. Hii ina maana kwamba unaweza kulipa bei kamili kwanza, kisha ukaomba urejeshewe sehemu ya fedha zako. Chaguo hizi hufanywa ziwe nafuu zaidi hasa kwa watu wenye kipato kinachostahili au kwa magari ya umeme yaliyotumika. Chaguo lolote utakalochagua, na tabia chache nzuri zinaweza kufanya safari zako ziwe safi na nafuu zaidi. Jipange mapema. Unganisha shughuli zako katika safari moja ili kuokoa muda na nishati. Endesha kwa utulivu. Kuongeza na kupunguza mwendo taratibu huongeza umbali wa gari la umeme, na huokoa mafuta kwenye magari mseto. Chaji usiku inapowezekana, kwa sababu mara nyingi umeme huwa nafuu zaidi wakati huo. Jaribu kutumia baiskeli au basi mara nyingi zaidi. Hata siku moja tu kwa wiki bila kutumia gari huleta akiba halisi, hupunguza hewa chafuzi, na hupunguza uchakavu wa gari lako binafsi. Tunza vifaa vyako. Kagua shinikizo la matairi, hudumia betri ipasavyo, na hifadhi baiskeli ya umeme ndani wakati wa majira ya baridi. Na mwisho, shiriki safari. Kupanga usafiri wa pamoja hupunguza uchafuzi wa mazingira na huimarisha uhusiano kati ya majirani na wafanyakazi wenzetu.