У нас вы можете посмотреть бесплатно 𝐒𝐄𝐊𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐆𝐀𝐈𝐑𝐎 - 𝐒𝐔𝐂𝐂𝐄𝐒𝐅𝐔𝐋 𝐒𝐓𝐎𝐑𝐘 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
"Video ni Documentary ya Successful Story ya Sekta ya Kilimo na Mazingira Gairo iliyotazamwa katika mkutano wa SACGOT uliokutanisha Wadau wa Kilimo, Mifugo na Mazingira mkoa wa Morogoro, na baadae kutazamwa katika Mkutano kama huo katika ngazi ya Taifa Gairo ni miongoni mwa Wilaya ambazo kiwango cha umasikini ni kikubwa sana na ndiyo maana, mimi na viongozi wenzangu tuliamua kuchukua hatua madhubuti kupitia Program ya 𝐔𝐫𝐢𝐭𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐣𝐚𝐧𝐢 𝐆𝐚𝐢𝐫𝐨 ambayo inagusa Sekta ya Kilimo (Mazao, Mifugo, Nyuki) na Sekta ya Mazingira. Tuliamua kuipa uzito Sekta ya Kilimo kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wamejiajiri kwenye sekta ya Kilimo, hivyo Sekta ya Kilimo Gairo ndiyo mhimili wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, hivyo jitihada za kuondoa umasikini haziwezi kuzaa matunda kama Sekta ya Kilimo haijakuwa na kuleta tija kwa mkulima. Hatuwezi kuendelea kuacha mkulima wa Gairo aendelee kuvuna Gunia 5 za mahindi au Gunia 3 za maharage kwenye ekari moja, badala ya kuvuna gunia 20 hadi 25 za mahindi au gunia 10 hadi 15 za maharage kwenye ekari moja. Pamoja na jitihada za kukuza sekta ya Kilimo, tuliamua pia kuweka mkazo katika Sekta ya Mazingira kwa sababu dunia hivi sasa imeshuhudia athari kubwa sana za mabadiliko ya Tabianchi kutokana na uharibifu wa Mazingira. Sekta ya Kilimo inaathirika kutokana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi hivyo Sekta hizi mbili lazima ziende sambamba. Shukrani kwa Kiongozi wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake wenye maono katika sekta hii. Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Adam Malima amekuwa mhimili mkubwa sana katika utekelezaji wa ajenda hii muhimu. Nawashukuru sana Viongozi wenzangu na wadau wote wa Sekta ya Kilimo hasa Maafisa Kilimo wote kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika Wilaya yetu ya Gairo" Jabiri O. Makame, Mkuu wa Wilaya ya Gairo