У нас вы можете посмотреть бесплатно DC NJOMBE AZINDUA HUDUMA KITUO CHA AFYA IWUNGILO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MKUU WA WILAYA NJOMBE AZINDUA HUDUMA KITUO CHA AFYA IWUNGILO Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe. Juma Sweda, amezindua kituo cha afya Kata ya Iwungilo Halmashauri ya Mji Njombe kitakacho wahudumia zaidi ya wakazi 10944. Akizungumza Disemba 01, 2025 mara baada ya kufungua kituo hicho Mkuu wa Wilaya Njombe amewataka wakazi hao kutumia kituo hicho kupata huduma za matibabu ya uhakika karibu na wananchi jambo ambalo litapunguza adhaa ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma kutoka maeneo mengine "Ningependa kupongeza Halmashauri ya Mji Njombe pamoja na uongozi mzima wa kijiji cha Iwungilo na kata kwa kutenga mapato ya ndani yatokanayo na shughuli za kilimo na ushuru wa miti na viazi kulipwa kwa wingi na kufanikisha ujenzi wa huu ,niombe tutumie Kituo cha Afya kwa kujipatia matibabu na uchunguzi wa afya zetu " alisema Mkuu wa wilaya Njombe. Aidha Mhe. Sweda amemtaka injinia amalizie kazi iliyobaki ya ukarabati wa hatua za mwisho kwenye jengo la mama na mtoto la Kituo hicho . Kituo cha Afya kata ya Iwungilo mpaka kuanza huduma kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 507 ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri na nguvu za wananchi zilizotumika katika kituo hicho. Ziara hiyo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, mganga mkuu halmashauri ya mji, wakuu wa idara Halmashauri ya Mji, Serikali ya kijiji cha Iwungilo na Kata ya Iwungilo.