У нас вы можете посмотреть бесплатно MAGU-Baraza la Madiwani lapitisha azimio la kuanzishwa kwa Wilaya mpya ya Kisesa. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ijumaa 15.10.2021. #Magu-mwanza Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoni Mwanza, limekutana katika kikao maalum chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Commrade Simon Mpandalume. Agenda kuu ikiwa ni kujadili mapendekezo ya kuanzishwa Wilaya mpya ya Kisesa. Baraza hilo limehudhuriwa pia na Mhe. Boniventula Destery Kiswaga Mbunge wa jimbo la Magu, awali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu Wilbard Bandola alitoa taarifa kuwa Halmashauri imepokea barua toka kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza yenye mwongozo, na rasmu ya kuanzishwa kwa Wilaya ya Kisesa. Akisoma Rasmu hiyo Wakiri wa Serikali Merchades Lusasa ameeleza Tarafa za Sanjo na Kahangara zikiwa na jumla kata 11 zimependekezwa kuunda Wilaya mpya, Huku Tarafa ya Itumbili na Ndagalu zenye jumla ya kata 14 zilipendekezwa kuunda Wilaya ya Magu(Wilaya mama). Baada ya Mjadala mwisho baraza liliazimia kuwa Tunakubaliana na kuanzishwa kwa Wilaya, lakini Kata moja ya Kahangaza ambayo ni jirani na makao makuu ya Wilaya ya Magu pale Ilungu, ibakie katika Wilaya ya Magu ili kuwasogezea huduma wananchi. Kwa Azimio hilo la Madiwani sasa Wilaya mama ya Magu itakuwa na kata 15, na Wilaya tarajani itakuwa na kata 10, Huku ikipendekezwa kuwa wanaweza kuzalisha kata zingine kwa kuzimega kata kubwa kama Mwamanga, Kisesa, Bujashi na Bukandwe. Baraza pia litoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi njema anayoifanya katika Taifa ikiwemo ya kutoa fursa kwa Wanamagu kuanzisha Wilaya mpya ya Kisesa. ‘KAZI IENDELEE’ Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Magu Habari, mawasiliano na itifaki. +255 716 094 601 dbubeshi@gmail.com