У нас вы можете посмотреть бесплатно Mh. Cecilia Paresso Atoa Mchango wa Milioni 2.5 Ujenzi Nyumba za Watumishi wa CCM Karatu или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Cecilia Daniel Paresso, ametoa mchango wa mbao zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu. Mbao hizo zimekabidhiwa rasmi leo mbele ya viongozi mbalimbali wa chama, wanachama pamoja na wadau wa maendeleo katika, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa awali wa kuunga mkono juhudi za chama katika kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mheshimiwa Paresso alisisitiza kuwa viongozi wanaotokana na CCM wana wajibu wa kuhakikisha wanajenga na kuimarisha chama chao ili kiendelee kuwa imara na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi. Alisema kuwa mshikamano, ushirikiano na kujitolea kwa viongozi pamoja na wanachama ni msingi muhimu katika kufanikisha miradi ya maendeleo ya chama, ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi ambao unalenga kuboresha ustawi wao na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. “Sisi kama viongozi tunaotokana na CCM tuna wajibu wa kujenga na kuimarisha chama chetu. Ni muhimu kila mmoja wetu kuendelea kushirikiana, kujitolea na kuchangia kwa kadiri ya uwezo wake ili kukifanya chama chetu kiendelee kuwa imara,” alisema Mheshimiwa Paresso. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Paresso pia aliwapongeza viongozi wa CCM Wilaya ya Karatu akiwemo mwenyekiti wa chama wilayani humo, viongozi wengine wa chama pamoja na Kamati ya Siasa kwa juhudi zao katika kusimamia na kuhamasisha ujenzi wa nyumba hiyo mpaka kufikia hatua iliyopo sasa. Aidha, aliwashukuru wanachama wa chama pamoja na wadau mbalimbali waliotoa michango yao ya hali na mali ili kuhakikisha ujenzi huo unasonga mbele. Mheshimiwa Paresso pia alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wote wa chama kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kuimarisha chama katika ngazi mbalimbali nchini. Kadhalika, alimpongeza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Kenani Kihongosi, kwa juhudi zake za kuimarisha uhai wa chama na kuendelea kukijenga katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kwa upande wao, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu walimshukuru Mheshimiwa Paresso kwa mchango wake huo wakieleza kuwa msaada huo utakuwa chachu muhimu ya kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo na kuwahamasisha wadau wengine kujitokeza kuchangia mradi huo. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Mheshimiwa Paresso ya kuendelea kushirikiana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuimarisha chama na kuleta maendeleo ndani ya Wilaya ya Karatu pamoja na Mkoa wa Arusha kwa ujumla. #CeciliaParesso #CCMKaratu #UjenziCCM #Arusha #SiasaTanzania