У нас вы можете посмотреть бесплатно Mwenyekiti wa Halmashauri Karatu na Wahisani Wakagua Barabara ya Selela Kuunganisha Karatu Monduli или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu District Mheshimiwa Engelbert Aloyce Qorro leo ameongoza ziara ya kikazi katika kijiji cha Selela kwa lengo la kukagua barabara inayotarajiwa kuunganisha Wilaya za Karatu na Monduli. Ziara hiyo ilifanyika pamoja na ujumbe wa wahisani wa maendeleo kutoka Praxis Tanzania Ltd wanaotathmini uwezekano wa kushiriki katika maendeleo ya miundombinu ya barabara hiyo muhimu. Mwenyekiti huyo na jopo lake walipokelewa katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Selela mbele ya Diwani wa Viti Maalum, Mwenyekiti wa Kijiji, pamoja na Watendaji wa Kata na Kijiji. Wananchi wa eneo hilo walijitokeza kwa wingi kuwapokea viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji Ndg Lomnyak, kwa niaba ya Diwani wa Kata ya Selela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mheshimiwa Kisiok Moitiko. Katika mapokezi hayo, wananchi walieleza furaha yao kubwa kwa ujio wa viongozi na wahisani hao, wakiamini kuwa ziara hiyo ni mwanzo wa matumaini mapya ya kufunguliwa kwa barabara hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ndoto ya wakazi wa maeneo hayo. Mmoja wa wananchi wa Selela alinukuliwa akisema: “Kwa miaka mingi tumekuwa tukitamani kuona barabara hii ikifunguliwa ili itusaidie kusafirisha mazao yetu na kurahisisha mawasiliano kati ya Monduli na Karatu. Leo tumefarijika sana kuwaona viongozi na wahisani wakifika hapa kujionea hali halisi ya eneo letu. Hii imetupa matumaini makubwa kuwa ndoto yetu inaweza kutimia. Baada ya mapokezi hayo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua barabara husika. Wananchi wa Selela kutoka Monduli kwa kushirikiana na wenzao wa Lostete walikuwa wameanza juhudi za kuifungua barabara hiyo ili iweze kupitika kwa vyombo vya moto badala ya kutumiwa na waenda kwa miguu pekee. Hata hivyo, jitihada hizo zilikwama kutokana na matumizi ya zana duni zisizoweza kumudu kazi hiyo pamoja na uwepo wa korongo kubwa la mto unaopokea maji kutoka eneo la Ngorongoro Conservation Area kuelekea Lake Manyara. Akizungumza na wananchi baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mheshimiwa Engelbert Aloyce Qorro aliwapongeza kwa moyo wao wa kujitolea kuanza kazi ya kuifungua barabara hiyo. Alieleza kuwa kuunganishwa kwa Wilaya za Karatu na Monduli kupitia barabara hiyo kutaleta manufaa makubwa kiuchumi kwa wananchi wa pande zote mbili. Alisisitiza kuwa barabara hiyo itakuwa njia muhimu ya kukuza biashara na shughuli za kijamii, sambamba na kuwa njia mbadala kwa watalii hasa wakati wa mvua pale Kirurumu River unapofurika na kuzuia upitaji wa kawaida. Aidha, alibainisha kuwa mradi huo unaweza kuvutia wawekezaji katika maeneo ya Mbulumbulu na Engaruka na hivyo kuongeza fursa za maendeleo kwa wananchi. Kwa upande wake, mwakilishi wa Praxis Tanzania Ltd Ndg Essau Peterson Pwelle alieleza kuwa walitembea umbali mrefu kwa miguu ili kujionea kwa karibu hali halisi ya eneo hilo na uwezekano wa kutoboa barabara hiyo muhimu inayounganisha Karatu na Monduli. Ndg Pwelle aliahidi kuwa mara baada ya kukamilika kwa ziara yao na kufuata taratibu zote za kidiplomasia na kitaalamu, wao kama wahisani watajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kusaidia juhudi za kufanikisha mradi huo. Alisisitiza kuwa endapo fedha za mradi zitapatikana, ni muhimu wadau wote kuweka mbele maslahi ya wananchi badala ya maslahi binafsi, jambo ambalo litafungua milango kwa wawekezaji zaidi kushiriki katika miradi mingine ya maendeleo. Ziara hiyo imeacha matumaini mapya kwa wananchi wa Selela, Lostete na maeneo jirani ambao kwa muda mrefu wamekuwa na ndoto ya kuona barabara hiyo muhimu ikifunguliwa ili kurahisisha usafiri, biashara na maendeleo ya kiuchumi kati ya Wilaya za Karatu na Monduli. #KaratuDistrict #MonduliDistrict #MaendeleoYaMiundombinu #BarabaraKaratuMonduli #UshirikianoWaMaendeleo