У нас вы можете посмотреть бесплатно Wakili: Geoffrey Mwambe Anatuhumiwa Kula Njama za Kumuua ‘Mkuu wa Polisi’, Uchochezi Mtandaoni или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam, Kisutu, Jumatatu, Desemba 15, 2025, ilikuwa imepanga kusikiliza shauri la maombi ya dhamana ya waziri wa zamani, Geoffrey Mwambe, aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Mwambe, ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mbunge wa Masasi (CCM), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, alikuwa anashikiliwa na Polisi tangu Desemba 7, 2025. Hata hivyo, kupitia wakili wake Hekima Mwasipu, Mwambe alifungua shauri la maombi ya dhamana Desemba 11, 2025, katika shauri la maombi namba 289778/2025, akiwataja wajibu maombi kuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZCO). Katika maombi hayo yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura, Mwambe aliomba mahakama iamuru afikishwe mahakamani na apewe dhamana kwa masharti yatakayowekwa na mahakama. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Wakili Mwasipu amesema kuwa mteja wake aliachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jana Jumapili Desemba 14, 2025, hali iliyofanya maombi yaliyokuwa yanasikilizwa leo kupoteza nguvu kisheria. Mwambe alikuwa anatuhumiwa kwa makosa mawili ya jinai, yakiwemo madai ya kutishia kumuua‘Mkuu wa Polisi’, ambaye hakutajwa jina, pamoja na tuhuma za uchochezi kupitia mitandao ya kijamii. Wakili Mwasipu ameongeza kuwa, licha ya kuachiwa kwa dhamana, Mwambe ataendelea kuripoti katika Ofisi ya ZCO wakati upelelezi ukiendelea, na endapo atabainika kuwa na kosa, hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani. You can follow us via; TWITTER: / thechanzo INSTAGRAM: / thechanzo FACEBOOK: / thechanzo TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_... Or visit our website: https://www.thechanzo.com Do you have news? contact us via Telegram/WhatsApp +255 753 815 105 The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.