У нас вы можете посмотреть бесплатно TRA MKOA WA MARA YATEKETEZA SIGARA,VIPODOZI, VIFAA TIBA VILIVYOINGIA KIMAGENDO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kitengo cha Forodha mkoani Mara, imeteketeza shehena kubwa ya bidhaa za magendo zikiwemo boksi za sigara, vifaa tiba, vipodozi na vifungashio, zenye jumla ya zaidi ya kilo 7,000. Operesheni hiyo imefanyika Januari 29, 2026 katika eneo la Nyabange, Wilaya ya Butiama, ambapo Meneja wa TRA mkoa wa Mara, Nasoro Ndemo, amesema bidhaa hizo zilikamatwa katika nyakati tofauti na mmiliki wake alitoroka mara baada ya kukamatwa. Meneja Msaidizi wa Forodha, Abdallah Mambi, amesema juhudi za kudhibiti uingizaji wa bidhaa haramu zinaendelea kuzaa matunda, huku elimu ikiendelea kutolewa kwa wafanyabiashara kufuata taratibu za kisheria. Akishuhudia zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Thecla Mchuchika, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amepongeza jitihada za TRA na kuonya kuwa yeyote atakayejaribu kukwepa kodi hatapona.