У нас вы можете посмотреть бесплатно MGANGA WA KIENYEJI AKUTWA AKIWA AMEFICHA JENEZA KWENYE KICHAKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
SHINYANGA: BAADHI ya wakazi wa mtaa wa Mwime Makungu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamepatwa na hofu baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kumalija Budeba ,55, anayedaiwa kuwa mganga wa kienyeji kuficha jeneza kwenye kichaka likiwa tupu eneo jirani na shamba lake na kuzuia watu kupita eneo hilo. Tukio hilo limejitokeza leo baada ya watu waliokuwa wakichunga mifugo kuliona jeneza hilo kisha kutoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa ambao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi. Kiongozi wa walinzi wa jadi wa mtaa huo, Someke John amesema baada ya kufika eneo la tukio walilazimika kulifungua ili kujiridhisha kama hakuna mwili wa binadamu kutokana na taarifa zilizo uwepo kuwa kuna mwili ndani ya jeneza hilo. "Tulipomhoji alikiri kufahamu uwepo wa jeneza hilo ambalo alikuwa akilitumia katika shughuli za sanaa, kuwa yupo msanii wake anaitwa Idd Masempele alikuwa analitumia katika matamasha yake ya muziki wa asili alilitelekeza katika eneo hili Julai mwaka huu,"amesema John. Mtuhumiwa amekiri uwepo wa jeneza hilo ambalo lilikuwa likitumiwa na msanii wa nyimbo za asili, Idd Masempele ambaye alimuita nyumbani kwake kumfundisha kijana wake sanaa ya muziki wa asili na alikuwa analitumia katika matamasha yake. Ofisa Utamaduni Manispaa ya Kahama Felix Ntibabara amesema hawajawahi kutoa kibali cha matumizi ya jeneza kwa ajili ya shughuli za sanaa za asili,na katika uwasilishaji wa maudhui ya nyimbo za asili ni kosa kutumia aina hiyo ya sanaa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kennedy Mgani amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kujua uhalali wake na jeneza hilo lililopo kituo cha polisi Kahama.