У нас вы можете посмотреть бесплатно Rais Samia: "Wanahaha kwa Uchu wa Madaraka na Ulwa'. Asisitiza Amani Kuelekea Uchaguzi или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Akizungumza katika Kongamano la Umoja wa Maimamu Tanzania, lilofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 24, 2025, Rais Samia ametahadharisha juu ya kupanda kwa joto la kisiasa wakati wa uchaguzi. “Kwa kawaida, kote duniani kipindi cha uchaguzi hupandisha joto la kisiasa nchini…..linatokea kwa sababu wapo wanaotafuta kutumia kipindi hicho kama mwanya wa kuvuruga amani, na hawa wako nje ya nchi na ndani ya nchi,” alieleza Rais Samia. “Nje ya nchi ni wale wanaohisi kwamba wakituvuruga yale wanayoyatamani kuyafanya ndani ya Tanzania tukivurugana pale watapata mwanya wa kuingia na kuja kuyafanya yale wanayoyatamani,” alifafanua zaidi. “Au labda watapata kubadilisha uongozi wa nchi, waje wale ambao hawakujengwa na misingi ile tuliyowekewa na wazee wetu waliotutangulia wakati wa uhuru. Waweke wao ambao wanaweza wakawaweka mawazo yao kichwani na wakaweza kuendeleza nchi kama wanavyofanya katika maeneo mengine,” aliongeza zaidi. “Lakini wale wa ndani kuna wawili wanaotumika na hao wa nje, lakini kuna wale ambao wanahaha kwa uchu wa madaraka na ulwa, ameomba amekosa, [anajiuliza] kwa nini nikose. Kwa nini yule na sio mimi, hao nao ni wavunjifu wa amani.” Unaweza kutufuatilia kupitia; TWITTER: / thechanzo INSTAGRAM: / thechanzo FACEBOOK: / thechanzo TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_... Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105 The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.