У нас вы можете посмотреть бесплатно TFRA YATOA MAFUNZO KWA MAAFISA KILIMO MOSHI DC или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), imetoa semina kwa Maafisa Kilimo wa wilaya, kata na vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwa lengo la kuboresha utoaji wa elimu sahihi kuhusu matumizi ya mbolea pamoja na uhuishaji wa taarifa za wakulima katika maeneo yao ya kazi. Semina hiyo imetolewa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa TFRA, Gothard Liampawe, ambaye amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maafisa kilimo na kuwapatia uelewa sahihi kuhusu namna mfumo wa taarifa za wakulima unavyofanya kazi ili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi. Amesema takwimu sahihi za wakulima ni muhimu katika kupanga mipango ya maendeleo ya sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati. “Tunapowajengea uwezo maafisa kilimo, tunahakikisha taarifa sahihi zinawafikia wakulima na pia serikali inapata takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga mipango ya kuboresha uzalishaji wa mazao,” amesema Liampawe. Kwa upande wake Mratibu wa Pembejeo za Ruzuku wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Hamza Mwinyihija, amesema halmashauri imejipanga kuhakikisha maafisa kilimo wanatoa elimu sahihi kwa wakulima kuhusu uhuishaji wa taarifa zao pamoja na matumizi bora ya mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao. “Ni wajibu wa maafisa kilimo kuwafikia wakulima katika maeneo yao na kuwapa elimu sahihi kuhusu matumizi ya mbolea na umuhimu wa kuhuisha taarifa zao ili waweze kunufaika na programu mbalimbali za serikali,” amesema Mwinyihija. Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya maafisa kilimo na wakulima utasaidia kuboresha mfumo wa usimamizi wa pembejeo na kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.